Joy FM

Wajawazito Kasulu watakiwa kutumia vizuri dawa za fefo na foliki

31 August 2026, 11:59

Mratibu wa kukabiliana na vifo vya mama na mtoto katika halmashauri ya Mji wa kasulu Bw, Kadslaus Rafael, Picha na Emmanuel Kamangu

Matumizi foliki na fefo kwa kufuata maelekezo ya mtaalamu wa afya husaidia kulinda afya ya mama na mtoto na kupunguza baadhi ya hatari wakati wa ujauzito.

Na Emmanuel Kamangu

Wanawake wajawazito katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu wametakiwa kutumia vizuri dawa  aina ya fefo pamoja na foliki  ambazo  husaidia kukua vizuri kwa viungo vya mtoto aliyeko tumbon.

Amebainisha hayo mratibu wa kukabiliana na vifo vya mama na mtoto katika halmashauri ya Mji wa kasulu Bw, Kadslaus Rafael ambaye amesema matokeo ya mjamzito  kujifungua mtoto mwenye mdomo sungura, mgongo wazi na wengine ubongo ukiwa nje ni kutokana na uhaba wa madini chuma ambayo yanapatikana katika dawa za Fefo ambazo waliowengi wamekuwa hawazitumii ipasavyo.

Aidha Bw, Rafael amesema wajawazito kufanya kazi ngumu wakati wa uzauzito pamoja na maambukizi ya njia ya mkojo ni moja ya mambo yanayosababisha kujifungua watoto njiti hivyo na kuwasihi kuhuzulia kiliki kwa wakati.

Redio joy imefanikiwa kuzungumza na mama anayeendelea na kiliki  Bi, Dayana Alfred ili kujua pengine ni kwanamuna gani wamekuwa wakifuata ushauri wa wataalamu juu ya namuna ya kutumia vema dawa wanazopewa akabainisha kuwa wengi wao wamekuwa hawajali huku wengine wakianza kiliki wakiwa na ujauzito wa kuanzia miezi sita jambo ambalo  amesema ni hatari kwa usalama wa mtoto alieko tumboni.

Hata hivyo lishe duni ,msongo wa mawazo,  uzito mdogo wa mama, upungufu wa Damu,ututaji wa sigara, unywaji wa pombe pamoja na uvutaji wa madawa ya kulevya ni moja ya sababu kubwa inayoweza kupelekea mjamzito kujifungua mtoto kabla ya wakati.

Sauti ya mwandishi wetu Emmanuel Kamangu