Joy FM

Askofu ataka familia kushirikiana katika maendeleo Kibondo

21 April 2026, 10:07

Waumini wa Kanisa la FPCT Kibondo mjini wa wkiwa katika ibaada, Picha na Dotto Josephati

Umuhimu wa familia kushirikiana kuleta maendeleo ni mkubwa sana katika maisha ya kijamii, kiuchumi na hata kirohona familia inapokuwa na mshikamano na ushirikiano, hujenga msingi imara wa mafanikio kwa kila mwanachama

Na Dotto Josephati

Askofu wa Kanisa la FPCT Kibondo ambaye pia ni mchungaji wa kanisa la FPCT Kibondo mjini mchungaji Buhimbi amewataka wanafamilia kufanya mambo yao kwa ushirikiano na mshikamano kwaajili ya maendeleo ya familia ili waweze kutimiza mipango yao ipasavyo.

Ameyasema hayo katika kilele cha wiki mwanamke ambayo ilianza April 13 hadi 19 ambapo amesema
familia ambayo Haina ushirikiano haiwezi kua na mafanikio.

Askofu wa Kanisa la FPCT Kibondo ambaye pia ni mchungaji wa kanisa la FPCT Kibondo mjini, Picha na Dotto Josephati
Sauti ya Mchungaji FPCT Kibondo

Vile vile mchungaji Buhimbi amewahimiza waumini wa kanisa Hilo kua na moyo wa utoaji Kwa hitaji ili
waweze kubalikiwa na kuongezewa zaidi.

Sauti ya Mchungaji FPCT Kibondo

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wanawake FPCT Jimbo la Kibondo Angesta Mishita ameeleza lengo la
kuwepo Kwa juma Hilo la Wanawake FPCT ambapo amesema juma hili linalengo la kuwakutanisha
wanawake kwaajili ya mafundisho na kufanya matendo ya huruma Kwa wenye uhitaji.

Waumini wa Kanisa la FPCT Kibondo mjini wa wkiwa katika ibaada, Picha na Dotto Josephati
Sauti ya Mwenyekiti wa Wanawake FPCT Jimbo la Kibondo Angesta Mishita

Hali kadhalika katika hitimisho la wiki mwanamke imeambatana na harambee kwaajili ya kutunisha
mfuko wa Wanawake ambayo utawasaidia kuakamilisha ujenzi ya nyumba yao Kwaajili ya shughuli za
Wanawake huku akiekeza namna fedhahiyo itakavyo wasaidia kutekeleza mipango yao

Sauti ya Mwenyekiti wa Wanawake FPCT Jimbo la Kibondo Angesta Mishita