Joy FM

Mwenge wa uhuru kumulika miradi ya maendeleo Kasulu

9 September 2025, 09:44

Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu, Picha na Hagai Ruyagila

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu amesema mwenge wa uhuru utetembelea na kuweka jiwe la msingi katika miradi ya maendeleo utakapowasili Wilayani humo

Na Hagai Ruyagila

Wananchi wilayani ya Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ambao unataraji kupokelewa wilayani humo septemba 17 mwaka huu.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Wilaya ya Kasulu, Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Isaac Mwakisu Amesema Mwenge wa uhuru utakimbizwa katika halmashauri zote za wilaya ya Kasulu kuanzia septemba 17 na 18 ambapo amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika meneo yote ambayo mwenge wa uhuru utatembelea na kuzindua miradi ya maendeleo.

Mbali na mwenge wa uhuru kanali Mwakisu pia amegusia umuhimu wawananchi kushiriki katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huu.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu
Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele, Picha na Hagai Ruyagila

Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele amesema katika kuiweka jamii pamoja wamekuwa wakifanya mabonanza mbalimbali lengo ikiwa ni kuhamasisha amani, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa wananchi.

Sauti ya Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele

Naye Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Sabinus Chaula amepongeza ushirikiano uliopo kati ya serikali na wananchi na ameahidi kuwa halmashauri hiyo itaendelea kushirikiana na wananchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Sauti ya Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Sabinus Chaula
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Sabinus Chaula, Picha na Hagai Ruyagila