Joy FM

Wadau wa maji wapendekeza bei mpya ya maji Kasulu

18 May 2026, 16:22

Baadhi ya wananchi na wadau wa maji Mjini Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Upatikanaji wa huduma bora ya maji ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla

Na Hagai Ruyagila

Wadau wa huduma ya maji katika halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma wamependekeza bei mpya ya bili ya maji kwa unit 1 kutoka shilingi 300 mpaka shilingi 500 na 1000 ili kuwasaidia wananchi kumudu gharama za kulipa huduma hiyo.

Bei ya sasa ya maji inayotumika kwa halmashauri ya Mji Kasulu ni shilingi 300 kwa unit 1 za maji ambayo imedumu kwa takribani miaka 23 tangu mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira kasulu ilipoanzishwa mwaka 2003 bei hiyo ilikuwa inakidhi mahitaji ya wananchi kwa wakati huo.

Baadhi ya wananchi na wadau wa maji Mjini Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kasulu Mjini (KUWASA) Mhandisi Samwel Kayombo anawasilisha kwenye kikao cha wadau wa maji kasulu mjini mapendekezo ya bei mpya za bili ya maji kutoka sh.300 hadi shilingi 3075 kwa unit 1 za maji.

Sauti ya Samwel Kayombo
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Kasulu mjini Mhandisi Samweli Kayombo, Picha na Hagai Ruyagila

Baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo mjadala ukaibuka miongoni mwa wadau wa maji Kasulu mjini.

Sauti ya Wadau wa maji

Kufuatia mjadala huo Uliodumu kwa zaidi ya saa 2:30 Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kasulu Sabinus Chaula akawakumbusha wajumbe kuwa hayo ni mapendekezo tu, nasiyo bei mpya.

Sauti ya Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kasulu
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Akifunga kikao hicho Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele amesisitiza kuwa kikao cha mwisho cha viongozi wa Serikali na wadau wa maji kitaamua na kupitisha rasmi bei mpya za bili za maji ambayo itaanza kutumika baada ya kupitishwa rasmi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 23 kupita.

Sauti ya Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele
Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele, Picha na Hagai Ruyagila