Joy FM
Joy FM
12 December 2025, 22:57

Serikali katika Manispaa ya Kigoma Ujiji imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kusogeza karibu huduma kwa wananchi
Na Mwandishi wetu
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Mkoani Kigoma wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo inayotekelezwa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Ziara hiyo imefanyika leo desemba 12, 2025 ikiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Kisena Mabuba huku akisema Manispaa inatekeleza miradi hamsini na Saba yenye thamani ya zaidi ya billion hamsini na tatu na miradi hiyo inayotokana na fedha kutoka Serikali kuu ni kiasi cha billion 51.6 na miradi ya mapato ya ndani ikigharimu zaidi ya bilioni 2.1.

Mkurugenzi huyo amesema ziara zitaendelea kwa makundi mbalimbali ya wananchi ili wapate kujua miradi inayoendelea kutekelezwa kutokana na Kodi na tozo zao.
Aidha mesema mara baada ya waandishi wa habari ziara nyingine itakayofuata ni pamoja na Viongozi wa Wafanyabishara, Viongozi wa dini na wazee maarufu ndani ya Manisoaa ya Kigoma Ujiji
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi unaoendelea wa shule mpya za awali na msingi Kata ya Kibirizi na Buhanda, Upanuzi wa Uwanja wa Ndege Kigoma, Ujenzi wa Kituo cha afya unaoendelea Rusimbi, Ofisi ya Kata ya Kasimbu, Ujenzi wa Barabara ya Bangwe -Ujiji.

Miradi mingine ni ujenzi unaoendelea wa daraja la mto Ruiche, Hospitali ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, shule ya Sekondari Mji Mwema, Ujenzi unaoendelea wa Ukumbi wa Kisasa eneo la Mwanga Community centre, Ujenzi wa soko la Kisasa la Mwanga na Ujenzi unaoendelea wa Jengo la Utawala.
