Joy FM

Familia ya kijana aliyefariki Kakonko yaomba uchunguzi ufanyike

16 November 2023, 17:03

Picha ya kijana anayedaiwa kufariki katika mazingira ya kutatanisha.

Familia ya Kijana Enock Elias aliyefariki katika mazingira ya kutatanisha yaomba uchunguzi dhidi ya waliohusika na mauaji hayo.

Na Kadislaus Ezekiel

Familia ya kijana Enock Elias Sabakwishi, mkazi wa kijiji cha Ilabiro kata ya Katanga wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, ambaye ameuwawa na kuzikwa katika mazingira ya kutatanisha imeomba serikali isaidie kwa haraka uchunguzi, kujua chanzo cha kifo cha kijana huyo na hatua zichukuliwe.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache tangu mwili wa kijana Enock Elias kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele, baada ya kuarifiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha kisha kukutwa amefariki.

Simanzi na majonzi yanaendelea nyumbani kwao na marehemu, ambapo mama mzazi pamoja na dada zake, wameomba uchunguzi ufanyike kwa haraka ili kujua chanzo cha kifo cha ndugu yao ili haki itendeke.

Sauti ya wanafamilia ambao wamefiwa na kijana wao

Wakati huohuo, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Zubery Kabwe, ameongozana na viongozi wengine wa chama hicho na kutoa pole, pamoja na kubeba ujumbe kwa mamlaka kufanya uchunguzi ili haki itolewe kwa familia hiyo.

Sauti ya Kiongizi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe

Hata hivyo ofisi ya mkoa wa Kigoma imeunda tume ya watu saba ili kufanya uchunguzi utakaokuja na majibu ya chanzo cha kifo cha kijana huyo, ambapo kaimu mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mlindoko amesema kamati hiyo itafanya kazi kwa hatua zote.

Sauti ya Kaimu Mkuu wa Mkoa Kigoma Mwanamvua Mlindoko