Joy FM

Mkandarasi aagizwa kuongeza kasi ujenzi barabara ya Uvinza

28 September 2023, 09:32

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya akiwa Mkoani Kigoma kukagua barabara ya Ilunde -Malagarasi Uvinza, Picha na Kadislaus Ezekiel.

Serikali imesema mkandarasi anayejenga barabara ya Ilunde – Malagarasi Uvinza kuwa amekiuka makubaliano ya mkataba wa kukamilisha na kukabidhi barabara ya ya Ilunde Uvinza Mwezi oktoba mwaka huu wa 2023.

Na, Kadislaus Ezekiel.

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amemwagiza mkandarasi anayejenga Barabara ya Malagarasi, Ilunde Uvinza kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 51.1, kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi, baada ya usuasua na kukiuka ukomo wa mkataba ambao unaelekeza akabidhi barabara hiyo mwezi oktober mwaka huu.

Akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua Barabara hiyo Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya amemwagiza mkandarasi kuongeza kasi ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma kwa kuendelea kutumia barabara za Vumbi na kukwamisha maendeleo.

Barabara ya Ilulunde – Malagarasi Uvinzi ikiendelea kujengwa, Picha na Kadislaus Ezekiel.

Awali akitoa Taarifa ya mradi, Mhandisi mshauri kutoka kampuni ya NORPLAN LIMITED Mhandisi Henry Ngogoloni amebainisha kasi ya utekelezaji kuwa ya kusuasua, wakati Meneja Tanroads mkoa wa Kigoma Mhandisi Narsi Choma akisema watamsimamia mkandarasi ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 51.1 inajengwa kwa thamani ya Bilioni 62.7, wakati mradi huo hadi sasa ukiwa umefikia asilimia 45 tuu ya utekelezaji.