Joy FM

Tanzania, Burundi kukabiliana na ajali Ziwa Tanganyika

30 August 2023, 12:52

Muonekano wa Mwambao wa Ziwa Tanganyika, Picha na Tryphone Odace

Katika kukabiliana na ajali ndani ya Ziwa Tanganyika Serikali ya Tanzania na Burundi zimeonyesha nia ya kushirikiana kutoa elimu ya matumizi ya vifaa vya usafirishaji ndani ya ziwa.

Na, Tryphone Odace

Nchi za Tanzania na Burundi zimeanza kuchukua hatua za kukabiliana na majanga ya ajali zinazotokea Katika Ziwa Tanganyika na kupelekea maafa na hasara kwa wananachi wa mataifa hayo, kwa kuhakikisha usalama wa vyombo vya usafirishaji vinakidhi ubora, ili kupunguza ajali majini.

Hayo yamejili wakati wa ziara ya ujumbe wa Burundi kupitia Shirika la Uwakala wa Meli kutembelea ujenzi wa utengenezaji wa meli na mbinu za kudhibiti changamoto zinazotokea wakati wa safari ima kwa meli au boti katika Ziwa Tanganyika.

Sehemu ya Ziwa Tanganyika Picha na Tryphone Odace

Mwakilishi  wa Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli  nchini Mozesi Mabamba  amesema suala la kuzingatia kati ya Tanzania na Burundi, ni kuona usalama wa abiria na malizao na vyombo vya usafirishaji kuwa na ubora unaotakiwa.

Mkurugenzi wa bandari na usafirishaji majini  kutoka Burundi Biherengede Jean amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Burundi katika masuala ya usalama majini.

Aidha Afisa Mfawidhi Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC mkoa wa Kigoma Abedi Mwanga, anawataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kwa njia ya maji kuhakikisha wanakuwa na vifaa vyote vya uokozi.