Joy FM

Vijana waliohitimu mafunzo JKT Bulombora watakiwa kuwa wazalendo

6 September 2023, 12:39

Mkuu wa Wilaya Kigoma Salum Kalli akiwa na Mkuu wa Kikosi cha JKT Bulombora pamoja na mwakilishi wa Mkuu wa majeshi, Picha na Tryphone Odace

Kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa JKT Bulombora kimesema kitaendelea kuwafundisha ujuzi na uzalendo vijana wote ili waweze kulitumikia Taifa.

Na, Tryphone Odace.

Vijana waliohitimu mafunzo ya kijeshi oparesheni miaka 60 katika kambi ya Jeshi la kujenga Taifa JKT, kikosi cha Jeshi 821 KJ Bulombora wametakiwa kuwa wazalendo katika kuilinda Nchi na kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa amani.

Haya yameelezwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Kanali Peter Lushika wakati wa kufunga mafunzo kwa vijana kwa mujibu wa sheria Operasheni miaka 60 ambapo amesema wanatakiwa kuendelea kuonyesha uzalendo kwa Taifa na kutojihusisha na vitendo viovu  kwenye jamii.

Mkuu wa Wilaya Kigoma Salum Kalli akiwa na Mkuu wa KJ Bulombora na Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi, Picha na Tryphone Odace.

Naye Mkuu wa kikosi cha 821 KJ Bulombora Luteni Kanali Juma Hongo  amesema mbali na vijana hao kupatiwa mafunzo mbalimbali wamewawezesha kupata stadi za maisha kupitia uzalishaji mali huku, Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Brigedia Jenerali Solotina Nshushi akiwataka kujiepusha na vitendo vitakavyohatarisha afya zao.

Mkuu wa Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT Bulombora Luteni Kanali Juma Hongo , Picha na Tryphone Odace.
Sauti ya Mkuu wa Kikosi Jeshi la kujenga Taifa Bulombora.

Awali wahitimu hao kupitia risala yao wamesema  kuwa mbali na kupatiwa ujuzi mbalimbali wameeeleza kambi hiyo inakabiliwa na changomoto za uhaba wa maji na umeme wa uhakika.

Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya Kigoma Salum Kalli amesema Serikali inaendelea kujivunia vijana hao kwani ni tunu kubwa katika kuhakikisha wanalinda nchi na atahakikisha anashughulikia changamoto hizo.