Joy FM

Prof. Ndalichako alipa deni kwa wananchi Kasulu

20 March 2024, 15:18

Waziri  ofisi ya waziri mkuu kazi , vijana , ajira na wenye ulemavu prof Joyce ndalichako amezindua magati matano ya maji katika mtaa wa nyachijima kata ya kigondo halmashauri ya mji wa kasulu ikiwa ni mwendelezo wa kuhakikisha serikali inamtua mama ndoo kichwani.

Akizindua mradi huo wa maji katika hafra ya wiki ya maji Duniani ndalichako  amesema wananchi wa mtaa wa nyachijima halmashauri ya mji wa kasulu wamekaa karibuni miaka 30 bila maji safi na salama jambo ambalo limekuwa likiwafanya kuugua magonjwa ya mara kwa mara na kushindwa kufanya shuguli zao za maendeleo huku akiahidi kuwa kata zote 15 za jimbo la kasulu mjini atahakiisha zinakuwa na maji ya kutosha.

Aidha Mkuu wa wilaya ya kasulu Kanali Isaac Mwakisu amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na miundombinu iliyopo ili miradi mbali mbali ya maji wilayani kasulu iweze kudumu.

Kwa upande wao baadhi ya wanawake wa mtaa wa nyachijima wameangua kilio cha furaha kutokana na kupitia madhira makubwa ya kutembea umbali mrefu jambo ambalo limekuwa  likipelekea changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ndoa zao kuteteleka.

Awali akisoma utekelezaji wa mradi huo Kaimu Mkurugenzi mtendaji  mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira halmashauri ya mji kasulu KUWASA Bw. Lema Jeremiah amesema kufikisha maji katika mtaa huo kumegalimu zaidi ya milioni 30 ikiwa ni mkakati wa Raisi Dk Samia suruhu hasan wa kumtua mama ndoo kichwani.