Joy FM

Shughuli za binadamu zaathiri uhifadhi wa wanyamapori Kigoma

5 April 2024, 13:51

Licha ya Serikali na wadau wa uhifadhi nchini kuhimiza utunzaji wa mazingira kwa lengo la kunusuru uhai wa viumbe vinavyoishi kwenye misitu imeelezwa kuwa bado shughuli za binadamu zimeendelea kuathiri uhifadhi wa wanyamapori ikiwemo sokwe.

Hayo yameelezwa na Mtafiti Dkt Zabibu Kabalika Kutoka Taasisi ya utafiti ya Jane Goodall wakati wa halfala kuadhimisha miaka 90 ya mwasisi wa taasisi hiyo ya Jane Goodall tangu kuzaliwa kwake iliyoambatana na ifaturi kwa watoto wa wanaoishi katika mazingira magumu kutoka kituo cha Sanganigwa.

Dkt. Zainabu amesema kuwa shughuli za kilimo na uchomaji moto misitu imeendelea kuwa kikwazo kwa wanyamapori ikiwemo sokwe na viumbe wengine.

Amesema kuwa ili kuhakikisha wanyama hao wanaishi, jamii na taasisi mbalimbali za uhifadhi wa mazingira kwa kushirikiana na serikali hawana budi kuendelea kuweka mikakati ya pamoja ili kuhakikisha uhifadhi endelevu unakuwepo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya Kigoma Mh. Salum Kalli amesema jitihada za Mtafiti huyo Dkt. Jane Gooadall zimesaidia Serikali katika kuongeza pato lakini kuitangaza Mkoa wa Kigoma kupitia hifadhi ya Gombe.Baadhi ya wadau wa mazingira akiwemo Mkurugenzi wa sayansi ya uhifadhi Shedrack Kamenya wamesema taasisi hiyo imeendelea kusimamia na kuendelea mawazo ya uhifadhi wa mazingira kupitia program mbalimbali na kwa mjibu wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo inalenga kuendelea kupanda miti nchi nzima kwa lengo la kuendelea utunzaji wa mazingi