Joy FM

Watoto wa miaka mitano hadi 14 kupatiwa dawa za minyoo na kichocho kigoma

22 November 2023, 10:17

Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Albert Msovela akiwa kwenye picha na viongozi baada ya kikao cha kuanza ugawaji wa dawa ya minyoo na kichocho, Picha na Tryphone Odace.

Imeelezwa kuwa jamii kushindwa kuzingatia usafi na kuwa na vyoo bora ni miongoni mwa sababu zinazosababisha kuendelea kusumbuliwa na magonjwa ya minyoo na kichocho.

Na Tryphone Odace

Jumla ya Watoto laki tano na tano elfu mia nane na arobaini wenye umri wa miaka mitano hadi kumi na nne wanatarajiwa kupatiwa dawa za minyo na kichocho katika Halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma.

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Bw. Albert Msovela  wakati akingumza na waandishi  wa habari juu ya kampeni hiyo ya utoaji wa dawa hizo ambapo amesema tayari maandalizi yamekamilika na lengo  ni kutokomeza magonjwa ya minyo na kichocho ambayo yamekuwa yakisumbua watoto.

Naye Mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele  Mkoa wa Kigoma Inocent Msikali amesema ukosefu wa vyoo bora kwenye jamii ya Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa sababu zinazosababisha uwepo wa magonjwa ya minyoo na kichoho kutokana na wengi wao kujisaidia vichakana.

Kwa upande wake, Mwakilishi Kutoka Wizara ya Afya Nashiri Abdallah amesema  dhamira ya Serikali ni kuhakikisha magonjwa yasiyopewa kipaumbele yanadhibitiwa ili yasiweze kuleta madhara makubwa kwa wananchi.

Mratu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele Mkoani Kigoma akieleza hali halisi ya magonjwa kichocho na minyoo, Picha na Tryphone Odace.

Wizara ya afya kupitia Mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wanapata kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza ambapo kwa mkoa wa Kigoma mara ya mwisho kutoa dawa za kichocho na minyoo ilikuwa mwa 2021.