Joy FM

Enabel yakabidhi madarasa yanayohamishika Kasulu

15 July 2026, 09:02

Baadhi ya vifaa vilivyomo kwenye madarasa hayo yanayohamishika, Picha na Hagai Ruyagila

Elimu ni msingi muhimu wa maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla na kupitia elimu, jamii hupata maarifa, ujuzi na maadili yanayochangia maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, utekelezaji wa miradi ya elimu unahitaji rasilimali nyingi, utaalamu na ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali

Na Hagai Ruyagila

Shirika la Enabel limekabidhi madarasa matatu ya kisasa yanayohamishika (Digitruck) kwa Serikali mkoani Kigoma yenye thamani ya shilingi milioni 600 yakiwa na kompyuta mpakato ili kuwawezesha walimu wa shule za Sekondari kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi.

Zoezi la kukabidhi madarasa hayo limefanyika katika kata ya Nyansha mjini Kasulu na yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali mkoani Kigoma washirika wa Enabel kutoka Nchini Kenya,Uganda na Rwanda.

Muonekano wa darasa linalohamishika ambalo ni miongoni mwa madarasa matatu yaliyikabidhiwa kwa serikali, Picha na Hagai Ruyagila

Mtaalamu wa kidigitali kutoka shirika la Enabel Walter John amesema mradi huo unalenga kuleta manufaa kwa waalimu na wanafunzi katika shule za sekondari.

Sauti ya Walter John
Mtaalamu wa kidigitali kutoka shirika la Enabel Bw.Walter John,Picha na Hagai Ruyagila

Mkurugenzi wa shirika la Enabel nchini Tanzania anayemaliza muda wake Geokint Koenraad amesema madarasa hayo yanayohamishika kwa kitalaamu Digitruck yamewekwa kwenye vituo vya rasilimali za walimu katika kata za Nyasha Halmashauri ya mji Kasulu Kata ya kizazi halmashauri ya wilaya ya Kibondo na kata ya Bitale Halmashauri ya wilaya ya Kigoma.

Sauti ya Geokint Koenraad

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro ambaye amewakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac mwakisu amezindua madarasa na vifaa hivyo nakukabidhi funguo kwa wakurugenzi wa Halmashauri zinazonufaika na mradi huo

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akimkabidhi funguo za darasa hilo la kidigital mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl Vumilia Julius Simbeye, Picha na Hagai Ruyagila

Nakueleza kuwa utakuwa na manufaa kwa jamii katika idara mbalimbali huku akisisitiza utunzaji wa vifaa hivyo.

Sauti ya Kanali Isaac Mwakisu
Baadhi ya Washiriki katika kuzindua mradi huo, Picha na Hagai Ruyagila

Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya wakurugenzi wa Wilaya ya Kibondo na wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Kasulu Mwl.Vumilia Simbeye amesema watasimamia vifaa hivyo na kuhakikisha vinaleta manufaa kwa wananchi,waalimu na wanafunzi.

Sauti ya Vumilia Simbeye
Mkuu wa Wilaya Kasulu akiwa kwenye picha na viongozi wa Enabel na Serikali, Picha na Hagai Ruyagila