Joy FM

Saratani ya mlango wa kizazi inatibiwa acheni imani potofu

22 April 2024, 09:30

Mwalimu akimweleza mtoto wwa kike kuwa saratani inatibika, Picha na Tovuti ya Buhigwe Dc

Ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi kwa watoto wa kike imeendelea kuwa tatizo jambo ambalo limeiamsha serikali kuendelea na kampeni ya chanjo kwa watoto wa kike ili kuepukana na ugonjwa huo

Na Emmanuel Kamangu – Buhigwe

Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma wanatarajia kutoa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa  mabinti elfu 23,982 wenye umri wa kuanzia miaka 9 hadi 14

Akizungumza na Redio Joy, Mratibu wa huduma za chanjo Wilaya ya Buhigwe  Stepphano Mambula amesema zoezi hilo linatarajiwa kuanzia tarehe 22 hadi 24 lengo ikiwa ni kukabiliana na ugonjwa wa saratini  ya mlango wa kizazi kwa mabinti wa kike.

Sauti ya mratibu wa huduma za chanjo Wilaya Buhigwe

Bw.Mabula amesema kwa kiasi kikubwa chanjo zinazoendelea kutolewa zimekuwa msaada mkubwa katika kuwakinga mabinti na maambukizi hasa kwenye via vya uzazi hivyo kuwataka wazazi kutowaficha wakati zoezi la chanjo litakapokuwa likiendelea.

Sauti ya mratibu wa huduma za chanjo Wilaya Buhigwe

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Wilaya ya buhigwe wameishukuru serikali kupitia idara ya afya kwa chanjo mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa kwa mabinti kwani zimekuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwemo ya uzazi.

Sauti ya wananchi wilayani Buhigwe na maoni juu ya chanjo ya saratani