Joy FM

EWURA yaonya uuzaji holela wa mafuta Kigoma

12 December 2024, 09:21

Meneja EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  mafunzo kwa wadau wa mafuta Wilayani  Kasulu, Picha na EWURA

Meneja wa mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji  EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher amewataka wadau wa masuala ya uuzaji wa mafuta kutumia fursa ya kuwekeza katika maeneo ya vijijini ambako kuna uhaba mkubwa wa vituo vya mafuta.

Na Kadislaus Ezekiel – Kasulu

Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Maji EWURA Kanda ya Magharibi inayojumusiha mikoa ya Tabora, Shinyanga, Katavi na Kigoma  imeonya uuzaji holela wa mafuta  ya vyombo vya moto katika madumu hasa maeneo ya vijijini na kuwa itawachukulia hatua kali za kisheria kutokana na  wafanyabiashara kutumia fursa ya uhaba wa vituo vya mafuta kuwekeza maeneo hayo.

Kwa sasa Mkoa mzima wa Kigoma kuna vituo 10 pekee vya mafuta maeneo ya vijijini, hali inayosababisha uwepo wa uhaba mkubwa wa mafuta na kuwalazimu  baadhi ya wananchi kufuata mafuta mjini na kuyauza kiholela bila kufuata kanuni na utalatibu.

Meneja EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher, akizungumza na wadau wa mafuta mjiniKasulu, Picha na EWURA

Meneja EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher anawataka wafanyabiashara kutumia frusa hiyo kuwekeza vituo vya mafuta kuepusha athari kwa jami na kuondokana na uuzaji huolela.

Mhandisi Christopher ametoa wito huo wakati wa mafunzo kwa wadau wa mafuta Wilayani  Kasulu yenye lengo la kuwejengea uwezo wa masuala ya kiudhibiti wadau wa sekta ndogo ya petroli kutoka mkoa wa Kigoma ukijumuisha washiriki kutoka wilaya zote sita za Kigoma, Kasulu, Kibondo, Kakonko, Buhigwe na Uvinza.

Sauti ya Meneja EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter Christopher

Kwa upande wao, baadhi ya wauzaji wa mafuta na wadau, wametoa maoni yao katika kufanikisha suala hilo na kuwa ni frasa katika kukuza uchumi.

Sauti ya baadhi ya wauzaji wa mafuta na wadau
Mwenyekiti wa wauzaji wa Mafuta wilaya ya Kigoma Bw.Salum Ally ,akizungumza  wakati wa mafunzo kwa wadau wa mafuta Wilayani  Kasulu Mkoani Kigoma, Picha na EWURA