Joy FM
Joy FM
15 August 2026, 11:46

Halmashauri ya Wilaya Kibondo Mkoani Kigoma imepongezwa kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi
Na Mwandishi wetu
Wajumbe wa jumuiya ya tawala za Mitaa Tanzania, ALAT Mkoa wa Kigoma wametakiwa kuendelea kishirikiana katika kufikia malengo ya kukuza maendeleo na uchumi wa halmashari za mkoa wa Kigoma.

Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Kigoma Bw. Alex Baragomwa amesema hayo wakati wa kikao cha jumuia hiyo cha kujadili na kupitia taarifa za robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026, kikao ambacho kimefanyika wilayani Kibondo
Baragomwa amesema ushirikiano wa wajumbe utasaidia kuinua uchumi wa halmashauri zote 8 za mkoa huo
Kabla ya kikao hicho, ALAT Mkoa wa Kigoma imeanza na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani Kibondo ambayo ni chuo cha maafisa tabibu, Soko jipya la kisasa la Nane nane, Jengo la halmashauri, vibanda vya soko la samaki pamoja na kikundi cha wajasiliamali cha Kaa kazi.

Hata hivyo wajumbe wa ALAT wameipongeza halmashauri ya wilaya ya Kibondo kwa ushirikiano ambao unafanyika katika kutekeleza miradi ya maendeleo
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Kanali mstaafu Aggrey Magwaza pamoja na Mweyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Kibondo Bw. Hamisi Tahiro wameipongeza jumuia ya ALAT kwa kuendelea kuimarisha ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ndani ya mkoa wa Kigoma.