Joy FM

Kamati ya fedha, uongozi na mipingo yakagua miradi Uvinza

28 September 2026, 21:11

Wajumbe wa kamati fedha, mioango na uongozi ikipokea taarifa katika moja ya miradi waliotembelea, Picha na Mwandishi wetu

Ukaguzi wa miradi hiyo ni hatua ya kujiridhisha na kuhakikisha usimamizi mzuri katika utekelezaji wa miradi hiyo

Na Mwandishi wetu

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha.

Akiongoza ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, Mh. Salvatory Motto, akiambatana na wajumbe wa Kamati hiyo, amekagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika Shule ya Msingi Chumvi, nyumba ya mwalimu katika Shule ya Sekondari Nyanganga, pamoja na ujenzi wa Vituo vya Afya Kazuramimba na Kandaga.

Viongozi mbalimbali wakiwa wamewasili katika moja ya miradi iliyotembelewa na kamati hiyo, Picha na Mwandishi wetu

Ziara hiyo imelenga kufuatilia hatua ya utekelezaji wa miradi, kubaini changamoto zinazoweza kuchelewesha ukamilishaji wake na kuweka mikakati ya kuzitatua, ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kamati imeeleza umuhimu wa kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo, kuhakikisha fedha na rasilimali zinazotengwa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na serikali.