Joy FM
Joy FM
23 October 2026, 15:33

Mchango wa sekta ya kilimo ni mkubwa katika uchumi wa nchi na ni muhimu kuwekeza katika sekta hiyo ili uwiano uwe sawa na sekta nyingine
Sadick Kibwana
Serikali Mkoani Kigoma imepanga kuyafikia makundi mbalimbali ya wakulima ikiwemo vyama vya Ushirika, mkulima binafsi na makampuni yanayojihusisha na Kilimo ili kuwawekea mazingira wezeshi yatakayokuwa na mchango thabiti katika dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.
Hayo yameelezwa na Afisa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Kilimo Tanzania TADB Mkoa wa Kigoma, Bw. Patrick Kapungu.

Aidha Kapungu ameongeza kuwa wamefika kwa baadhi ya wilaya za mkoa wa kigoma na kuwa watahakikisha wanawafikia watu wote.
Kwa upande wao, baadhi ya wakulima kutoka Wilaya za Kigoma na Buhigwe wamesema kuenea kwa huduma za kibenki ndiyo mwanzo wa kupata maendeleo ya kweli ya kilimo nchini.
TADB imeendelea kushuka hadi ngazi za vijiji na kata ili kutoa elimu ya mikopo nafuu iwafikie wakulima wengi nchini, kwa ajili ya kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya 2050.