Joy FM
Joy FM
6 November 2026, 20:42

Msaada huo unatajwa kupunguza upungufu wa madawati katika Shule hiyo huku uongozi wa shule hiyo ukitakiwa kutunza samani hizo ili ziweze kufanikisha lengo lililokusudiwa
Na Hagai Ruyagila
Kampuni ya CR CONSORTIUM, kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kupitia mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), imetoa msaada wa madawati 25, meza 10 na viti 10 kwa Shule ya Msingi Mumnyika iliyopo katika Halmashauri ya Mji Kasulu, mkoani Kigoma.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya samani hizo, Mwakilishi wa Meneja wa Mradi wa TRC kipande cha saba na nane, kinachotoka Uvinza hadi Msongati, Mhandisi Julius Oliver, amesema msaada huo umetolewa kufuatia uhitaji na upungufu wa samani hizo katika shule hiyo.

Amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi za kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za kijamii.
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Luteni Kanali Joseph Murimi, amewataka viongozi wa shule hiyo kuhakikisha msaada huo unatumika ipasavyo ili kuwa na tija katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Aidha, amezihimiza taasisi na mashirika mengine kuendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia jamii na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mumnyika Gerion Ngowi amesema walikuwa na changamoto ya madawati hivyo msaada huo unakwenda kupunguza changamato ya madawati katika shule hiyo.
