Joy FM

RC Kigoma ataka vyama vya ushirika kuwa waadilifu

20 August 2026, 17:06

Mkuu wa Mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro, Picha na Josephine Kiravu

Zao la tumbaku ni moja ya mazao makuu ya biashara katika mkoa wa Kigoma ikiwaingizia kipato wakulima wengi hasa katika wilaya za Kasulu, Kakonko na Uvinza

Na Josephine Kiravu

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amevitaka vyama vya ushirika kuwa waadilifu ili kuendelea kukuza uzalishaji wa zao la tumbaku ambapo kwa mwaka 2025/2026 lilishika nafasi ya pili kwa ngazi ya mkoa kwa kuingiza zaidi ya shilingi bilioni 5 katika pato la mkoa.

Hayo yamejiri wakati wa kikao cha bodi ya Tumbaku ambapo wadau wamepata nafasi ya kujadili na kutafuta suluhu ya changamoto zinazowakabili wakulima wa zao hilo.Na hapa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dinna Mathamani anasema ni vyema viongozi kuelekeza nguvu kutoa elimu kwa wakulima ili kuzalisha kwa wingi zao hilo.

Mkuu wa Mkoa wa akiwa kwenye kikao cha bodi ya kahawa, Picha na Josephine Kiravu

Kwa upande wake, Afisa mazingira bodi ya Tumbaku Elisha Chao amesema kwa msimu wa kilimo 2024/2025 nchi imeweza kuzalisha dola za kimarekani milioni 475 kutokana na zao la tumbaku, na kwa sasa wanaendelea kudhibiti wanunuzi wasio waaminifu kwa kutowapa leseni ili kuendelea kumnufaisha mkulima.

Na hapa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma akatoa maelekezo kwa viongozi wa bodi na vyama vya ushirika kuhakikisha mkulima ananufaika kupitia kilimo hicho huku akisisitiza pia wakulima kufuata utaratibu wa kukata miti wanapohitaji kuni kwa ajili ya kukausha tumbaku.

Mkuu wa Mkoa wa akiwa kwenye kikao cha bodi ya kahawa, Picha na Josephine Kiravu

Zao la tumbaku ni moja ya mazao makuu ya biashara katika mkoa wa Kigoma ikiwaingizia kipato wakulima wengi hasa katika wilaya za Kasulu, Kakonko na Uvinza hata hivyo wakulima wanakumbana na changamoto za mara kwa mara kama vile kushuka kwa bei za zao hilo na upatikanaji wa pembejeo.

Mmoja wa wadu akizungumza katika kikao cha wadau wa tumbaku, Picha na Josephine Kiravu