Joy FM

Mwenge wa uhuru waridhishwa na mradi wa maji Luhuru Kakonko

8 September 2026, 01:16

Muonekano wa mradi wa maji Luhuru Wilayani Kakonko, Picha na Mwandishi wetu

Mradi wa maji Luhuru uliopo Wilayani Kakonko unaenda kuwa mwarobaini ya ukosefubwa maji kwa wananchi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za maji

Na Mwandishi wetu

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Wazo Mwang’onda ametoa wito wa kuendelea kutunzwa miundombinu ya maji ili iweze kudumu na kutoa huduma kwa muda mrefu.

Kiongozi huyo ametoa wito huo mara baada ya kukagua utekelezaji wa mradi wa visima vitano vya Maji katika Kijiji cha Luhuru wilayani Kakonko.

Kiongozi wa mbio za mwenge Luhuru akiwa katika tenki la maji lililopo kijiji xha Luhuru, Picha na Mwandishi wetu

Amesema miradi ya maji inayotekelezwa katika maeneo ya vijiji na mijini ni dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu katika kuhakikisha anamtua mama ndoo kichwani.

Mradi huo wa Maji unatekelezwa na Serikali kwa Thamani ya Shilingi 358,197,905.

Muonekano wa mradi wa maji Luhuru Wilayani Kakonko, Picha na Mwandishi wetu

Baadhi ya wakazi wanaonufaika na Mradi huo wamesema kwa sasa wanapata maji safi tofauti na hapo awali ambapo walikua wakitegemea kupata huduma hiyo kutoka kwenye visima na maeneo ya mabondeni.