Joy FM

Mbunge atoa milioni 2.5 kusaidia mama asiyekuwa nyumba

14 September 2026, 09:44

Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini Nuru Kashakari akiwa kwenye picha na mama alipatiwa msaada fedha ya kujenga nyumba pamoja mwenyekiti wa kijiji cha Ruchugi, Picha na Orida Sayon

Wananchi wa Kijiji cha Ruchugi Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma wamesema kuwa hatua za mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini kujitoa kwa ajili ya wananchi wake kutokana na namna ambavyo ameendelea kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali

Na Orida Sayon

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini, Mhe. Nuru Kashakari, ametoa kiasi cha shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya kumsaidia  mama asiye na makazi ya kuishi baada ya nyumba yake kuuzwa na mme wake na mtoto mchanga aliyekosa maziwa ya mama kutokana na mama yake kuwa na matatizo ya afya akili.

Msaada huo ulitolewa wakati wa mkutano wa Mbunge huyo na wananchi uliolenga kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kata ya Uvinza mkoani Kigoma.

Katika mkutano huo, wananchi waliwasilisha kero mbalimbali, ikiwemo changamoto ya mtoto mchanga aliyezaliwa na mama mwenye changamoto za afya ya akili, pamoja na mama ambaye amekuwa akiishi bila kuwa na makazi kwa muda mrefu.

Akizungumzia changamoto hizo, Mhe. Kashakari, maarufu kwa jina la Kandahali, aliamua kutoa zaidi ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia wahitaji hao.

Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini Nuru Kashakari akiwa kwenye picha na mama alipatiwa msaada fedha ya kujenga nyumba pamoja mwenyekiti wa kijiji cha Ruchugi, Picha na Orida Sayon

Kati ya fedha hizo, sehemu yake itatumika kusaidia ujenzi wa makazi ya mama huyo ambaye alikuwa akikabiliwa na ukosefu wa nyumba ya kuishi, huku sehemu nyingine akinunua maziwa kwa ajili ya mtoto mchanga aliyekosa maziwa ya mama kutokana na mama yake kuwa na matatizo ya afya ya akili.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruchugi, Ramadhan Said Kayungilo, alieleza kwa undani mazingira na changamoto zilizochangia mama huyo kukosa makazi ya kuishi kwa muda mrefu kutokana na nyumba yake kuanguka na kushindwa kujenga nyingine.

Aidha, wananchi waliopokea msaada huo walimshukuru Mbunge Nuru Kashakari kwa hatua yake ya kuwasaidia, wakieleza kuwa msaada huo utawasaidia kukabiliana na changamoto walizonazo na kuboresha maisha yao.

Msaada huo ni sehemu ya juhudi za Mbunge huyo katika kusikiliza kero za wananchi na kuchukua hatua za kuzitatua, hususan kwa wananchi walio katika mazingira magumu.

Mbunge wa jimbo la Kigoma kusini Nuru Kashakari maarufu Kandakhari, Picha na Orida Sayon