Joy FM

Wazazi na walezi watakiwa kulea watoto katika maadili Kasulu

24 August 2026, 13:47

Baadhi ya wanafunzi, Picha na Hagai Ruyagila

Malezi bora kwa watoto ni msingi imara kwa maisha yao ya baadaye

Na Hagai Ruyagila

Wazazi na Walezi katika Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kuwalea watoto wao katika misingi ya maadili mema, ili waweze kuwa na mwenendo mzuri, kuheshimu jamii na kuwa viongozi bora wa baadaye.

Wito huo umetolewa na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Nurfus Aziz Ndee, wakati wa mahafali ya darasa la saba na kidato cha nne yaliyofanyika katika shule za Hekima na Agape zilizopo Mjini Kasulu.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu, Nurfus Aziz Ndee, Picha na Hagai Ruyagila

Amesema malezi bora yanapaswa kuanzia nyumbani, kwa kuwa mtoto anayelelewa katika misingi ya maadili mema ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kitaaluma na kuwa raia mwema mwenye mchango chanya katika maendeleo ya jamii.

Sauti ya Nurfus Aziz Ndee

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa shule za Hekima na Agape Sekondari, Fedia Yared, amesema ili mtoto afanye vizuri kitaaluma na kuwa na maadili mema, mzazi anapaswa kuhakikisha anampatia mazingira bora ya malezi na kumpeleka katika shule inayoweza kumsaidia kupata elimu bora pamoja na malezi yanayozingatia maadili.

Mkurugenzi wa shule za Hekima na Agape sekondari Fedia Yared, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Fedia Yared

Pia ameiomba serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa malezi ya watoto, ili wazazi na walezi kufahamu wajibu wao na kufuatilia kwa karibu mwenendo wa watoto wao.

Sauti ya Fedia Yared

Baadhi ya wazazi na walezi walioshiki katika sherehe za mahafali hayo wamesema kujenga urafiki na watoto ni muhimu na humsaidia mtoto kuwa huru kuzungumza na mzazi wake kuhusu changamoto mbalimbali, jambo linaloweza kumsaidia kufanya vizuri kitaaluma na kudumisha maadili mema.

Sauti ya Wazazi na Walezi
Baadhi ya wazazi na walezi waliohudhuria katika mahafali hayo, Picha na Hagai Ruyagila