Joy FM

Serikali yatoa pikipiki 4 kwa maafisa ugani Kigoma

12 January 2024, 08:28

Serikali imetoa pikipiki 4 zenye thamani ya shilingi Milioni 12 kwa maafisa ugani wa idara ya mifugo na uvuvi katika Manispaa ya Kigoma ili kurahisisha kufanya kazi ya kutoa Elimu kwa wafugaji, wakulima na wavuvi ili wazalishe kwa tija.

Na Lucas Hoha

Akigawa pikipiki hizo kwa maafisa hao, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli amewaomba maafisa hao kuzitumia vizuri pikipiki hizo  kwa kwenda maeneo ambayo yalikuwa hawafiki ili kutoa Elimu kwa wavuvi na wafugaji ili iwasaidie kuinua uchumi.

mkuu wa wilaya Salum Kalli

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Lessi Majala amesema serikali dhamira ya kutoa pikipiki hizo ni kutaka kuongeza motisha  kwa watumishi wa halmashauri ili kuwatumikia wananchi na kuleta matokeo chanya yatakayosaidia kuondoa umasiki kwa wananchi.

Sauti ya Lessi Majala

Kwa upande wao, baadhi ya maafisa ugani ambao wamepatiwa pikipiki hizo wamesema awali walikuwa wanafanya kazi kwenye mazingra magumu katika kuwafikia wananchi na kuwa kwa sasa watafanya kazi itayoleta maendeleo kwa wananchi.

maafisa Ugani

Pikipiki hizo ni sehemu ya Pikipiki zilizotolewa na serkali kuu kwa lengo la kuzigawa kwa  maafisa kilimo na uvuvi lengo likiwa kuwafikia wananchi kwa urahisi.