Joy FM

Bilioni 3 kujenga ofisi mpya za wilaya Kibondo

25 January 2024, 15:16

Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imeanza ujenzi wa ofisi mpya za halmashauri hiyo zitakazogharimu zaidi ya shilingi  bilioni 3 mpaka kukamilika kwake ikiwa ni mikakati ya serikali ya kuboresha mazingira ya kutolea huduma kwa wananchi.

Muonekano wa jengo la ofisi linaloendelea kujengwa kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma. Picha na james Jovin

Na, James Jovin

Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Daniel Ndarangavye akimwakilisha mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo katika ziara ya kitaifa ya jumuiya ya umoja wa vijana ccm.

Daniel Ndarangavye

Kwa upande wake, kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Steven Janks amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo mpaka sasa umefikia asilimia arobaini na kwamba tayari zimepokelewa fedha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji.

Naye kaimu mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana cmm taifa bi. Rehema Sombi amemshukuru raisi Samia Suluhu Hassani kwa kutenga fedha za ujenzi wa jengo hilo ambalo litakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa wilaya ya Kibondo.