Joy FM

Wanachuo Kasulu wakosa vifaa vya kujifunzia

25 April 2024, 14:49

Nembo ya chuo cha ualimu Kasulu mkoani Kigoma

Serikali imeombwa kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kujifunzia wanafunzi wa chuo cha ualimu kaslu Mkoani Kigoma.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Chuo cha Ualimu Kasulu (Kasulu TTC) kilichopo halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma kinakabiliwa na changamoto ya vifaa vya kufundishia hali inayopelekea wanachuo kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao yakiwemo masomo ya sayansi

Ni katika awamu ya 38 mahafari ya 39 ya chuo cha ualimu Kasulu ambapo katika risala iliyosomwa na rais mstaafu wa serikali ya wanachuo Bw. Zabron Njamajame amesema mbali na mafanikio ambayo wameyatapa amezitaja pia baadhi ya changamoto hizo kuwa zinakwamisha ufaulu kwa wananchuo.

Sauti ya wanachuo wakieleza changamoto zinaazowakabili

Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo cha ualimu Kasulu Zawadi Ngereja amesema wanachuo hao wameandaliwa vizuri na wamejengewa uwezo wa kutoa elimu kwa jamii ili kuwaandaa vijana wenye uwezo wa kuliongoza taifa.

Sauti ya makamu Mkuu wa chuo cha ualimu kasulu

Naye mgeni rasmi katika mahafari hayo Meneja wa NMB wilaya ya Kasulu ndugu. Ipyana Mwakatobe amesema atazifanyia kazi changamoto zote zinazowakabili wanachuo hao.

Sauti ya Meneja wa Benki ya NMB

Jumla ya wananchuo wa kada mbali mbali ambao wamehitimu ni 266 kutoka ngazi tofauti ambapo wanawake ni 125 na wanaume ni 141