Joy FM
Joy FM
8 August 2024, 09:38

Serikali ya Tanzania na Burundi zimeendelea na zoezi la kuhamasisha wakimbizi waliopo kwenye kambi za wakimbizi mkoani ili kuweza kurejea nchini burundi kutokana na amani ilipo kwa sasa nchini humo.
Na Kadislaus Ezekiel – Kasulu
Wakimbizi wa nchi ya Burundi waliowahi kuhifadhiwa mkoani kigoma na mikoa mingine nchini, wamewataka wakimbizi ambao bado hawajarejea burundi, kuchukua hatua za haraka kwa hiyari kurudi kujenga nchi yao na kuwahakikisha uwepo wa amani tele kwa raia wote wa nchi ya burundi.
Wakiwa katika zoezi la kuhamasisha wakimbizi wa burundi kurejea nchini mwao, baadhi ya wakimbizi ambao tayari wamerejea wameeleza amani na usalama kuimarika na kutoa wito kwa ndugu zao, kurudi kujenga nchi ya burundi kwa pamoja.
Akihutubia mamia ya wakimbizi wanaohifadhiwa kambi ya nyarugusu Naibu waziri wa mambo ya ndani, maendeleo ya jamii na usalama wa raia wa burundi brigedia jenerali nibona bonansize amewahakikisha uwepo wa amani kwa watu wote wanaorejea nchini burundi.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa tanzania mheshimiwa daniel sillo ambaye ameambatana na ujumbe wa viongozi wa nchi ya burundi amewataka wakimbizi kutoendelea kurithisha na ukimbizi kwa watoto wao na kusisitiza kurejena mara moja.