Joy FM

Askofu Bwatta ahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura serikali za mitaa

11 November 2024, 12:09

Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta, Picha na Hagai Ruyagila

Zikiwa zimesalia siku chache kufanyika kwa uchaguzi wa serkali za mitaa hapo novemba 27 mwaka huu, wananchi wametakiwa kujitokeza kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa srikali za mitaa.

Na Hagai Ruyagila – Kasulu

Wananchi wilayani Kasulu mkoani Kigoma waliojindikisha kwenye daftari la mkaazi wametakiwa kwenda kupiga kura ifikapo septemba 27 mwaka huu ili kuwapata viongozi bora watakao waletea maendeleo katika maeneo yao.

Akizungumza na radio joy fm Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta amesema mfumo wa nchi ni wakidemokrasia hivyo lazima wananchi wapige kula ili kuwapata viongozi bora.

Amesema ni haki kwa kila aliyejiandikisha katika daftari la mkaazi kutumia fursa hiyo kwenda kupiga kura wakati utakapofika.

Sauti ya Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta

Aidha Askofu Bwatta amesema siasa ni mfumo wa maisha ya kila siku japo wapo baadhi wanaochafua siasa kwa kushindwa kutimiza ahadi zao walizo waahidi wananchi.

Pia amewaomba wasisimizi wa uchaguzi kusimamia vyema mchakato mzima wa uchaguzi ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza.

Sauti ya Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Western Tanganyika Mhashamu Emmanuel Bwatta

Nao baadhi ya wananchi kutoka wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wamesema wako tayari kupiga kura na kuchagua viongozi ambao watasimamia vyema shughuli za maendeleo na kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Sauti ya baadhi ya wananchi kutoka wilayani Kasulu Mkoani Kigoma