Joy FM

Serikali kutambua mchango wa mabaharia katika ukuaji wa uchumi Kigoma

18 June 2026, 13:30

Mkuu wa Mkoa Kigoma akizungumza na waandishi wa habari, Picha na Tryphone Odace

Serikali imesema itaendelea kusimamia sera, miongozo na mikataba ya kimataifa katika kushughulikia na kutatua changamoto za mabaharia Nchini

Na Tryphone Odace

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, amewataka wananchi pamoja na wadau wa usafiri majini kushirikiana na serikali katika kuimarisha usalama wa usafiri majini na ustawi wa mabaharia nchini.

Balozi Sirro amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimishi ya siku ya mabaharia duniani ambayo kitafaifa yatafanyika Mkoani Kigoma na kuwa serikali imeendelea kutambua mchango wa mabaharia katika usafirishaji wa majini ambao umekuwa ukichochea maendeleo ya uchumi wa taifa.

Naye Kaimu Meneja wa Mafunzo na utoaji vyeti kwa mabaharia kutoka shirika la uwakala wa meli Tanzania TASAC Mhandisi Lameck Sondo amesema maadhimisho hayo yanalenga kutoa elimu kwa wananchi na mabaharia ili kutambua namna ya kujiokoa na kutekeleza sera na miongozo ya usafirishaji majini katika ushaghuli zao.

Mkuu wa Mkoa Kigoma akiwa na viongozi wa TASAC na malaria, Picha na Tryphone Odace

Kwa upande wake Hassan Mbarouk kutoka Mamlaka ya usafiri baharini Zanzibar amesema katika kuhakikisha changamoto na maslahi ya mabaharia zinatatuliwa serikali imeendelea kusimamia sheria ya utekelezaji wa mikataba ya kimataifa katika kuhakikisha mabaharia wanapata haki zao.

Siku ya mabaharia duniani huadhimishwa June 25 ya kila mwaka na nchi wanachama wa shirika la baharia duniani IMO kwa lengo la kutambua mchango wa mabaharia katika usafirishaji wa majini na mwaka huu madhimisho hayo yamebeba kaulimbiu isemayo kutoka sera hadi utekelezaji, kuimarisha ubora katika sekta ya usafiri majini.