Joy FM

Ekari 400 kugawiwa kwa wananchi wanaoishi maeneo yasiyo rasmi

9 May 2024, 12:34

Mkuu wa wilaya kasulu akizungumzia ugawaji wa maeneo kwa ajili ya wananchi kuhama maeneo yasiyo rasmi, Picha na Michael Mpunije

Kutengwa kwa eneo hilo huenda ikawa mwarobaini wa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na mamlaka za serikali hasa wakala wa misitu tanzania TSF ambayo imekuwa kwenye migogoro na wananchi wanaovamia maeneo ya hifadhi.

Na Michael Mpunije – Kasulu

Serikali wilayani Kasulu mkoani Kigoma imetenga eneo la zaidi ya ekari 400 kutoka katika hifadhi ya wanyamapori katika kitalu cha katoto kata ya Kagera nkanda ili kuwahamisha wakazi wa katoto ambao wanaishi katika maeneo yasiyo rasmi.

Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Kasulu kanali Isaac mwakisu wakati akizugumza na wananchi wa Kata ya kagera nkanda halmashauri ya wilaya ya Kasulu.

Muonekana wa mashamba ya wakulima katika pori la hifadhi ya kagerankanda, Picha na Kasulu Dc

Kanali mwakisu amesema serikali imelenga kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi ili kurahisisha shughuli za maendeleo kufanyika huku akiwataka viongozi wa vijiji kusisitiza matumizi bora ya Ardhi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya kasulu kanali mwakisu akizungumza na wananchi wa kagerankanda

Kwa upande wake Kamishina wa Ardhi TFS wilaya ya Kasulu bw. Paulo mauton Ngoshora amewataka wananchi kuwa makini na baadhi ya watu wanao wachangisha hela kwa njia ya utapeli kwa madai kuwa wanagawa ardhi kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo.

Sauti ya kamishna wa ardhi TFS wilaya ya kasulu

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Kagera nkanda bw.Ntamusano Nyandura amesema atahakikisha anasimamia na kutunza kikamilifu maeneo hayo ili shughuli za wananchi ziweze kufanyika kwa uhuru kwa ajili ya maslahi ya taifa.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha kagerankanda