Joy FM

Wasichana elfu 30 kupewa chanjo saratani ya mlango wa kizazi Kibondo

23 April 2024, 11:32

Chanjo ya HPV ikichangnywa tayari kuwachanja wasichana wilayani Kibondo, Picha na James Jovin

Viongozi wa ngazi za vijiji na kata wameshauriwa kusimamia na kuhamasisha wazazi na walezi kuwapa nafasi watoto wa kike kupewa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.

Na James Jovin – Kibondo

Idara ya afya katika halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma imelenga kutoa chanjo ya saratani ya shingo ya mlango wa kizazi kwa wasichana zaidi ya elfu thelathini  wenye umri wa miaka 9 mpaka 14 ikiwa ni mkakati wa kuendelea kudhibiti ugonjwa huo unaosambaa kwa kasi kote nchini.

Hayo yamebainishwa na afisa chanjo wa wilaya ya Kibondo bw. Malili Malugu wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi kilichoketi ili kujadili mikakati ya kufanikisha zoezi hilo kote wilayani humo.

Bw. Malili amesema kuwa katika wilaya ya Kibondo chanjo hiyo imekuwa ikitolewa tangu mwaka 2018 hivyo ikiwa ni wiki ya chanjo kitaifa idara ya afya imelenga kuchanja wasichana zaidi ya elfu thelathini ambao hawakuchanjwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Sauti ya mratibu wa chanjo wilaya kibondo

Kwa upande wake mganga mkuu wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo Dr. Henry Chinyuka amewataka wanawake kujenga mazoea ya kupima magonjwa ya saratani mara kwa mara ili waweze kupatiwa matibabu ya mapema hasa kwa watakaokutwa na magonjwa hayo.

Sauti ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kibondo

Afisa tarafa wa tarafa ya kifura bw. Shekarata Omary akimwakilisha mkuu wa wilaya ya kibondo kanali Agrey Magwaza  katika kikao hicho amewataka wadau mbali mbali wa kamati ya afya ya msingi kufikisha elimu kwa jamii ili zoezi hilo liweze kufanyika kwa mafanikio.

Sauti ya afisa tarafa kifura wilaya ya kibondo