Joy FM

Wafanyabiashara soko la Gungu walia na ukosefu wa miundombinu bora

14 December 2023, 16:19

Sehemu ya miundombinu ya mifereji kando na soko la Gungu yakiwa yamejaa maji. Picha na Tryphone Odace

Serikali imeombwa kukarabati miundombinu ya barabara na mitaro inayopita katika soko la Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma.

Na Orida Sayon.

Wafanyabiashara wa soko la Gungu lililoko kata ya gungu maniapaa ya kigoma ujiji wameitaka serikali kuboresha miundombinu ya barabara na mitalo ili kuthibiti athari zinazotokana mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali mkoani kigoma.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wafanya biashara wakati wakizungumza na radio joy fm, na kueleza madhara yanayotokana na ubovu wa miundombinu iliyopo katika kata ya gungu hasa maeneo yanayozunguka soko hilo ikiwemo uharibifu wa bidhaa zao

Naye katibu wa soko la gungu, bw. fadhili mbogo ameitaka manispaa ya kigoma ujiji, ameomba Serikali kutekeleza ahadi zinazotolewa kwa wananchi ili kuhakikisha miundombinu bora kwa soko la gungu inaimarishwa kwani wafanya biashara wengi wanatumia soko hilo kujipatia kipato.

Kwa upande wake diwani wa kata ya gungu bakari rajabu  ameeleza kuwa hali ya barabara na mitalo katika kata ya gungu sio rafiki kwa wakazi na wafanya biashara huku akiitaka serikali kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini, tarura kuangalia upya namna ya kuboresha miundombinu  kwani kata hiyo inabeba maji yanayotiririka kutoka kata nyingine ndani ya manispaa.