Joy FM

ACT Wazalendo yampitisha zito kuwa rais

6 May 2024, 17:06

Viongozi wa chama cha ACT Wazalendo wakiwa katika pich ya pamoja, Picha na mtandao

Kiongozi wa cha ACT wazalendo Zitto Zuberi Kabwa amesema kama atagombea urais mwaka 2025 kama wananchi na wanachama wa chama hicho watampa ridhaa ya kuwaongoza.

Na Kadislaus Ezekiel – Kigoma

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa chama cha  ACT WAZALENDO Taifa Othumani Masoud, amewataka wafuasi wa chama hicho na watanzania, kukiamini chama hicho na kukipa lidhaa ya kushika dora, na kusisitiza uwepo wa tume huru ya uchaguzi.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Othumani Masoud, amesema hayo wakati wa maadhimisho ya miama kumi ya chama hicho yalifanyika mjini kigoma.

Sauti ya makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya zanzibar

Kwa upande wao viongozi mbalimbali wa chama hicho, akiwemo mwenyekiti wa ACT WAZALENDO mkoa Kigoma Kizza Mayeye, ameitaka serikali kuboresha maisha ya watanzania, Wakati  kiongozi mkuu mstaafu  wa ACT WAZALENDO Zitto Kabwe, akieleza nia yake ya kugombea uraisi kama akipewa lidhaa na chama hicho.

Sauti ya viongozi wa chama cha ACT wazalendo

Hata hivyo baadhi ya wafuasi wa chama hichi wamekitaka chama hicho kusaidia kutatua changomoto zinawakabili wananchi ikiwemo ziwa Tanganyika kufungwa hali wanataja kuwa huenda ikaathiri uchumi wa wananchi.