Joy FM

Jamii yatakiwa kuzingatia maadili

4 August 2023, 10:09

Wajumbe wa kamati ya maadili Mkoa wa Kigoma wakiwa na Katibu wa Sekretarieti ya maadili,Picha na Josephine Kiravu

Maadili nchini yanaonekana kuendelea kuporomoka hali inayosababisha jamii kuendelea kupotoka na kusababisha jamii kuwa katika hali ngumu ya maisha hasa kufanyiwa ukatilii.

Na, Josephine Kiravu

Jamii Mkoani Kigoma imetakiwa Kujiepusha vitendo vilivyo kinyume na maadili ya Kitanzania kuanzia ngazi ya familia,Taasis za Umma na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ili kulinda kizazi Kijacho katika Nyanja mbalimbali Nchini

Rai hiyo imetolewa na Katibu msaidizi Kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya maadili na Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Gerad Mwaitebele akiwa katika mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Kigoma 

Katibu msaidizi Kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya maadili na Viongozi, Picha na Josephine Kiravu

Mwaitebele Amesema Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayo nafasi katika kuelimisha jamii kuendeleza na kudumisha Uzalendo, Maadili na Kuchukia maovu ikiwa ni pamoja na kumsaidia mwananchi kufikisha malalamiko yao .

Sauti ya Katibu msaidizi ofisi ya rais Sekretarieti ya maadili

Kwa upande wao baadhi ya wadau kutoka Taasis mbalimbali zisizo za kiserikali akiwemo, wamesema Utandawazi na wasanii wa sanaa hasa ya muziki na maigizo wamechangia kwa kiasi kikubwa kuharibu maadili kwenye jamii nchini.

Wajumbe wa mkutano wa Sekretarieti ya maadili Mkoani Kigoma, Picha na Josephine Kiravu
Sauti ya wadau wa masuala ya ukatilii kigoma

Mkutano wa mwaka wa mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani Kigoma ambao umeanza hspo Jana unatarajia kufikia tamati hapo kesho huku suala la maadili na uwazi likiendelea kusisigizwa na viongozi mbalimbali akiwemo Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Kigoma.