Joy FM

Wananchi wametakiwa kununua vipodozi kwenye maduka yaliyoruhusiwa

18 July 2023, 11:23

Kaimu Meneja wa Kanda ya Magharibi TBS, Bw. Rodney Alananga akiongea na wafanyabiashara wa Vipodozi wa mkoa wa Kigoma, Picha na TBS.

Shirika la viwango Tanzania TBS limesema litaendelea kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaouza bidha zilizopigwa marufuku ili kuepusha matumizi ya vipodozi visivyokidhi viwango kutumika kwa wananchi.

Na, Lucas Hoha

Wananchi Mkoani Kigoma wametakiwa kununua vipodozi kwenye maduka ambayo yameruhusiwa na wahakikishe kama vipodozi hivyo vina nembo  ya TBS, ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtumiaji ikiwemo kupata Kansa ya ngozi.

Wito huo umetolewa na Meneja wa Shirika la Viwango Tanzania TBS Mkoa wa Kigoma Rodney Alananga wakati akizungumza na kituo hiki akiwa Ofisini kwake ambapo amewaasa wananchi kuuliza na kupata taarifa sahihi za kipodozi kabla ya kuvitumia, huku akitaja baadhi ya vipotozi ambavyo vimepigwa mafuruku.

Baadhi ya Washiriki wa mafunzo yaliyotelewa na TBS Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Picha na TBS.
Sauti ya Meneja wa TBS kanda ya Magharibi

Aidha Alananga amekemea tabia ya baadhi ya watu ambao sio waaminifu wanaoingiza nchini  vipodozi  ambavyo vimepigwa  marufuku na serikali  kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria huku akianisha baadhi ya adhabu ambazo mtu atakumbana nazo pindi akikamatwa .

Sauti ya Meneja wa TBS Kanda ya Magharibi.

Kwa upande wao baadhi wananchi wa Mkoa wa Kigoma ambao ni watumiaji wa vipodozi wamekiri kutokuwa na uelewa wa kutambua vipodozi ambavyo nisahihi kwa matumizi na ambavyo siyo sahihi.

Sauti ya Wananchi Mkoani Kigoma wanaotumia vipodozi