Joy FM

Halmashauri ya Kasulu mji yafikia lengo la utoaji wa chanjo ya polio

27 September 2023, 12:20

Mratibu wa chanjo Halmashauri ya Mji Kasulu Bi. Itumbi Munisi, Picha na Hagai Ruyagila

Chanjo ya Polio hutolewa kwa watoto ili kuwakinga na magonjwa ya polio kwa watoto walio chini ya miaka nane.

Na, Hagai Ruyagila

Halmashauri ya mji Kasulu mkoani kigoma imefanikiwa kuvuka lengo kwa asilimia 128 katika utoaji wa chanjo ya polio ya matone kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8 iliyoendeshwa kwa muda wa siku nne.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Chanjo halmashauri hiyo Itumbi Munisi wakati akizungumza na Radio Joy fm katika kituo cha afya Kiganamo ambapo amesema wamevuka lengo walilokuwa wamejiwekea la kutoa chanjo ya polio kwa watoto 86,760.

Sauti ya Mratibu wa Chanjo Halmashauri ya Kasulu Mji.

Aidha Munisi amewaomba wazazi na walezi kuwa na mwamko wa kuitikia chanjo kwa ajili ya watoto wao kwani mtoto anaposhindwa kupata chanjo hii itasababisha kupata ulemavu au kifo.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi wamesema  ni vyema  kila  mzazi akaona umuhimu wa  kumpeleka  mtoto wake kupatiwachanzo ya polio ya matone kwani haina madhara yoyote kulingana na walivyo elekezwa na wataalamu wa afya 

Utoaji wa chanjo ya polio ya matone kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8 ulianza mnamo septemba 21 -24. 2023 na wameongeza siku nyingine mbili ili kuhakikisha wale ambao hawakuwa wamefikiwa kupata chanjo hiyo wanafanikiwa.