Joy FM

Wanafunzi 600 hawajaripoti shule wilayani kibondo

9 February 2024, 13:56

Baadhi ya wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza kibondo na hawajaripoti wakiwa wamekamata katika msako unaoendelea, Picha na James Jovin.

Ofis ya Eliu wilayani Kibondo imeanza msako wa kuwatafuta wanafunzi waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza na hawajaripoti shuleni mpaka sasa.

Na, James Jovin

Ni ripoti ya Mwandishi wetu James Jovin

Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imeanza msako wa wanafunzo wote ambao bado hawajajiandikisha kuanza masomo ya kidato cha kwanza ikiwa ni zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu shule zilipofunguliwa. 

Akizungumza na Radio Joy wakati wa msako huo afisa elimu wa shule za Sekondari wilayani Kibondo bw. Julius Kakyama amesema kuwa zaidi ya wanafunzi 600 hawajaripoti kuanza masomo ya kidato cha kwanza mpaka sasa. 

Aidha amesema kuwa zoezi hilo limeanzia katika kata za Busagara na Busunzu ambapo wazazi wa watoto hao hukamatwa na kuhojiwa ili waweze kueleza sababu za watoto wao kushindwa kuanza masomo licha ya kwamba ni haki yao ya msingi.

Sauti ya afisa elimu Halmashauri ya Wilaya Kiboondo

Baadhi ya wazazi waliozungumza na radio Joy wamebainisha kuwa umasikini na kukosa mahitaji ya msingi ni miongoni mwa sababu kubwa inayosababisha watoto wao kushindwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza

Licha ya kubainisha kuwa umasikini ndio chanzo kikubwa cha wanafunzi kuacha kwenda shule lakini pia baadhi ya wanafunzi walionekana kuwa wamefundishwa kukataa wakidai kuwa hawapendi shule swala hilo lilipingwa vikali na mkurugenzi mtendaji bw. Deocles rutema 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza amesema kuwa kusoma ni haki ya mototo hivyo kila mzazi anapaswa kutimiza wajibu wake kabla ya sheria na hatua zaidi za kinidhamu kuchukua mkondo wake. 

Mkuu wa Wilaya Kibondo Kanali Agrey Magwaza, Picha na James Jovin