Joy FM

TAKUKURU yabaini mapungufu kwenye miradi 25 ya maendeleo Kigoma

1 February 2024, 09:25

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru mkoani Kigoma imebaini mapungufu kwenye miradi 25 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 9 iliyofuatiliwa katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2023.

Na, Lucas Hoha

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kigoma John Mgallah wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma kuhusu utendaji kazi wa Takukuru.

Mgalla ametaja baadhi ya mapungufu hayo ikiwemo vifaa visivyokidhi viwango kutumika kwenye miradi ya maendeleo.

Aidha katika kipindi hicho Takukuru wemetembelea kata 17 za Mkoa wa Kigoma na kuibua kero 166 ambapo kero 149 kati ya hizo zimeshatatuliwa kero nyingine zilizotolewa na wananchi ni ubovu wa miundombinu ya umeme, migogoro ya ardhi, migogoro ya mipaka katika vijiji vya mwakizega na katete, huduma hafifu za upatikanaji wa maji safi na salama, Polisi, Biashara na Utawala.

Aidha katika upande wa uchunguzi na mashitaka Takukuru Mkoa wa Kigoma imepokea jumla ya malalamiko 54 ambapo malalamiko 31 kati ya hayo hayakuhusu rushwa.

Mbali na hayo Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wametakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Takukuru kwa Kuliona jukumu lakuzuia na kupambana na rushwa ni la kila mmoja kwa kuzingatia kauli mbiu isemayo kuzuia rushwa ni Jukumu lako na langu, tutimize wajibu wetu.