Joy FM

TRA Kigoma yakamata bidhaa feki

2 May 2024, 11:26

Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa kigoma Deogratius Shuma, Picha na Luca Hoha

Serikali kupitia mamlaka ya mapato imewataka wananchi na wadau mbalimbali ili kusaidia kukabiliana na wimbi la uingizwaji wa bidhaa feki Nchini.

Na Lucas Hoha – Kigoma

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA, Mkoa wa kigoma imekamata bidhaa mbalimbali ikiwemo vipodozi na vinywaji ambavyo vimeingizwa nchini kinyume na sheria kupitia  mpaka wa Burundi na Tanzania  licha ya baadhi ya bidhaa kupigwa marufuku kuingia nchini na shirika la viwango Tanzania TBS.

Hayo yamebanishwa na Meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa kigoma Deogratius Shuma wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu bidhaa hizo ambazo zimekamatwa katika wilaya ya buhigwe mkoani kigoma zikitokea nchini Burundi.

Baadhi ya maafisa wa TRA kigoma wakikagua mzigo wa bidha ulioingia nchini kinyume cha sheria, Picha na Lucas Hoha

Bw. Shuma amesema bidhaa hizo hazikupita kwenye mpaka rasmi kwa lengo la kukwepa kulipa Kodi, huku akiwaomba wananchi kuacha kufanya biashara haramu kwani zinasabisha hasara kwa wananchi na serikali.

Sauti ya Meneja TRA mko wa kigoma

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa mamlaka hiyo wamesema kwa mjibu wa sheria zilizopo bidhaa zinapokamatwa wanashirikiana na taasisi nyingine ikiwemo TBS kubaini ni bidhaa zipi zinafaa kwa matumizi na zile ambazo hazifai zinateketezwa kwa moto.

Baadhi ya viongozi wakizungumzia suala la bidhaa fekikuingia nchini

Nao baadhi ya wananchi kutoka mataifa yote mawili yaani Tanzania na Burundi wakizungumza na kituo hiki wakiwa katika kata ya Munanila Wilaya ya buhigwe mkoani kigoma  wamekemea tabia ya wananchi kuingiza bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine kinyume na sheria kwani baadhi ya bidhaa hizo hasa vipodozi  hazina sifa kwa matumizi na vimekuwa vikisababisha  madhara kwenye ngozi.

Bidhaa feki zilizokamatwa na TRA mpakani mwa Tanzania na Burundi, Picha na Lucas Hoha
Sauti ya wananchi wa eneo la mnanila buhigwe wakizungumzia bidhaa feki