Joy FM
Joy FM
14 October 2026, 13:26

Wakati Burundi ikiendelea na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 baadhi ya vyama vya upinzani ikiwemo Frodebu vimeonyesha nia ya kususia uchaguzi
Na Bukuru Daniel
Chama cha upinzani cha Sahwanya-FRODEBU nchini Burundi kimetangaza kutoshiriki uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika Mei 3, 2027, kikisema kuwa hakuna kidemokrasia inayoashiria kuwa utakuwa wa huru,haki na wa kuaminika.
Baraza la kitaifa la uongozi la chama hicho, baada ya kutathmini maandalizi ya uchaguzi. FRODEBU inadai kuwa dosari zilizopo zinaweza kusababisha matokeo yanayofanana na yale ya uchaguzi wa wabunge na viongozi wa serikali za mitaa uliofanyika Juni 2025.
Katika taarifa yake, chama hicho kimesema mazungumzo na serikali, wizara ya mambo ya ndani na tume huru ya taifa ya uchaguzi hayajazaa matokeo yanayotoa matumaini ya mabadiliko katika mchakato wa uchaguzi.

FRODEBU imesema itaendelea kuhamasisha wanachama wake kudai uchaguzi wa uwazi na wa kuaminika, huku ikiwaelekeza kujiandaa kwa uchaguzi wa wabunge na serikali za mitaa wa mwaka 2030.
Uamuzi huo unakuja wakati chama tawala cha CNDD-FDD tayari kimemteua Rais Évariste Ndayishimiye kuwania muhula mwingine.
Wakati huohuo, chama cha CNL kinakabiliwa na mgogoro wa uongozi kati ya makundi yanayohusishwa na Agathon Rwasa na Nestor Girukwishaka.
Hata hivyo, madai ya FRODEBU kuhusu dosari za uchaguzi ni msimamo wa chama hicho, na taarifa iliyochapishwa haijatoa tathmini huru ya madai hayo.