Joy FM

Vijana wa JKT Bulombora wametakiwa kuwa wazalendo kwa Taifa

11 July 2023, 13:39

Naibu Kamanda wa kikosi cha Jeshi la wananchi 24 Meja Heri Mbuma akizungumza wakati wa sherehe za miaka 60 ya JKT, Picha na Kadislaus Ezekiel.

Vijana wa Kikosi cha Jeshi la kujenga Taifa JKT Bulombora kilichopo Mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kuwa wazalendo kwa kulitumikia Taifa na kulinda amani ya Nchi.

Na, Kadislaus Ezekiel

Jeshi la Kujenga Taifa JKT, kikosi cha Jeshi 821 KJ Bulombora Kimesema kitaendelea Kuzalisha Vijana wenye nidhamu ya kulitumikia Taifa, uzalendo wa kutunza amani na kushiriki katika uzalishaji mali.

Naibu Kamanda kikosi cha Jeshi 24 Meja Heri Mbuma amesema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la kujenga Taifa, JKT ambapo ameeleza  kuwa JKT ni chombo imara cha kusaidia vijana wa kulitumikia Taifa.

Sauti ya Naibu Kamanda wa Kikosi cha 821 JKT Bulombora Meja Mbuma

Kaimu Kamanda kikosi 821 KJ Bulombora Luteni Rashidi Kiliza amesema katika kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa JKT kikosi hicho kimeshiriki katika shughuli za kijamii ikiwemo usafi na kupanda miti maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma.

Baadhi ya Askari wa Jeshi la wananchi JWZ pamoja na wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 60 ya JKT katika kamibi ya Bulombora, Picha na Kadislaus Ezekiel
Sauti ya Kaimu ya Kamanda wa kikosi cha 821 Bulombora Luteni Rashid Kiliza

Baadhi ya Vijana wanaopata mafunzo ya Kijeshi katika kambi hiyo wamepongeza hatua zinazochukuliwa na JKT Kwa kuwajengea uwezo wa kutambua majukumu ya kulitumikia Taifa na kujiepusha na makundi ya uvunjifu wa amani.

Vijana wa JKT Bulombora wakiwa wametulia kusikiliza hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa sherehe za miaka 60 ya JKT, Picha Kadislaus Ezekiel.
Sauti ya Vijana wa JKT Bulombora Kigoma