Joy FM

Ujasiriamali kuwaponza walimu Kibondo

24 April 2024, 15:02

Baadhi ya walimu katika shule ya msingi Boma wilayani Kibondo mkoani Kigoma kwa kushirikiana na kamati ya shule hiyo wanatuhumiwa kuwazuwia wajasiliamali wadogo kuuza bidhaa zao kando na shule hiyo na badala yake walimu ndio wamegeuka wafanyabiashara badala ya kufundisha wanafunzi.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa kitongoji cha Nankuye bwana Nuhu Msafiri wakati wa kikao cha kusikiliza kero za wananchi kilichoitishwa na mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza katika kitongoji hicho.

Mwenyekiti wa kitongoji : Nuhu Msafiri

Bi. Martha Minja pamoja na  Aurelia James ambao ni wajasiliamali wadogo jirani na shule hiyo wamesema walimu wamekuwa wakilazimisha wanafunzi kununua bidhaa zao huku wakiwachapa viboko wale wanaobainika kwenda kununua chochote sehemu nyingine

wajasiriamali

Bi. Neema Miti akimwakilisha mkurugenzi mtendaji katika kikao hicho cha kusikiliza kero za wananchi amesema kuwa changamoto hiyo itafikishwa katika vikao vya nidhamu ili kuweza kujadilia swala hilo kwa utekelezaji na usuluhishi kati ya walimu na wajasiliamali hao.

Mwakilishi wa mkurugenzi: Bi Neema Miti