Joy FM

CCM Kigoma kupitia UWT yalia na vitendo vya ukatili

24 October 2023, 21:20

CHAMA cha Mapinduzi CCM, kupitia umoja wa wanawake Tanzania UWT mkoa wa Kigoma, kimeraani na kukemea vitendo vya ukatili vinavyofanyika kwa watoto na wanawake, nakuomba jamii kuungana pamoja kukemea vitendo hivyo na kuripoti katika mamlaka husika ili kuchukua hatua mara moja inapobainika Mtu au Watu Kufanya Vitendo hivyo.

Baadhi ya wanawake wakifanya usafi katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Wanawake Tanzania, Picha na Tryphone Odace

Hayo yamebainika wakati wa maadhimisho ya  Wiki ya Umoja wa wanawake wa Tanzania UWT Mkoa wa Kigoma, ambapo mwenyekiti wa umoja huo mkoa wa Kigoma Agripina Buyogela, amesema ni wajibu wa kila mtanzania kukemea vitendo vya ukatili ili kuwa na ustawi bora wa watoto na wanawake nchini.

Mwenyekiti UWT : Agripina Buyogela

Aidha Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania UWT mkoa wa Kigoma Sara Kairanya ameoimba jamii kwa ujumla kuthamini na kujali watoto kwa kupinga ukatili dhidi yao, wakati Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Kigoma, Rashidi Simindu akisihi vijana kujiepusha na vitendo vinavyotokana na utandawazi ambayo vimeharibu vijana wengi