Joy FM
Joy FM
29 April 2026, 12:11

Vikundi 13 vya walemavu vimepatiwa mkopo kati ya vikundi 23 ambavyo vimepatiwa mkopo wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko katika robo ya pili ya mwaka wa fedha wa 2025/2026
Mkopo huo umetolewa ikiwa ni mkakati wa serikali wa kuviwezesha vikundi vya walemavu kati ya vikundi vya wanawake na vijana ambapo vikundi hivyo vimepata milioni 51 kati ya milioni 106 zilizotolewa.

Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Kakonko Bw. Mustapha Mtungwe amesema vikundi vingine ambavyo vimepatiwa mkopo ni vikundi 10 vya wanawake na vijana na mkopo huo ukawe chachu ya kukuza uchumi.

Naye mratibu wa mikopo idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Kakonko Bi. Safia Mjuberi amewataka wanavikundi kutekeleza miradi yao kulingana na malengo ambayo walijiwekea wakati wa kuomba mkopo