Joy FM

Wanafunzi wapatiwa msaada wa pazia Buhigwe

16 April 2026, 4:52 pm

Wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wakati wakikabidhiwa msaada wa mapazia, Picha na Michael Mpunije

Shule ambayo haina madirisha, mapazia bado yanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha mazingira ya kujifunzia kwani yanaweza kuwa na umuhimu hata kwa shule ambayo haina madirisha, ingawa mara nyingi huonekana kama yanahitajika zaidi kwenye madirisha.

Na Michael Mpunije

Umoja wa Wananchi wa kata ya Mwayaya wanaoishi katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam wametoa msaada wa pazia 24 zenye thamani ya shilingi laki tano (500,000) kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Manyovu, iliyopo Kata ya Mwayaya, Wilayani Buhigwe Mkoani kigoma

Msaada huo umetolewa ili kusaidia kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa madirisha katika baadhi ya vyumba wanavyotumia wanafunzi wanaoishi bweni shuleni hapo, hali ambayo imekuwa ikiathiri mazingira yao ya kujifunzia na kuishi.

Akikabidhi vitu hivyo kwa niaba ya wanamwayaya waishio mikoa ya pwani na Dar es salaam Diwani wa kata ya mwayaya Ephraim Sibanganya mwakeye ameeleza kuwa lengo la msaada huo ni kuboresha ustawi wa wanafunzi na kuwapatia mazingira bora zaidi ya kujifunzia huku akiwasisitiza kuongeza bidii katika masomo.

Sauti ya Diwani
Wanafunzi wa shule ya sekondari Manyovu iliyopo Wilayani Buhigwe, Picha na Michael Mpunije

Awali, Mkuu wa Shule ya Sekondari Manyovu, Mwalimu Najimu ahmad mpendq alieleza kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa madirisha  katika vyumba vya wanafunzi wanaoishi bweni, hali inayosababisha ukosefu wa faragha kwa wanafunzi ambapo licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na uongozi wa shule, bado kuna uhitaji mkubwa wa maboresho ya miundombinu ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira salama na rafiki kwa ajili ya kujifunza na kuishi.

Sauti ya Mkuu wa shule

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Manyovu wameushukuru Umoja wa wana Mwayaya kwa msaada wa pazia walioutoa.

Wakisema kuwa msaada huo umesaidia kuboresha mazingira ya malazi shuleni hapo, hasa kwa kuwakinga na upepo na baridi kali na kuwapatia faragha wakiwa vyumbani, hali itakayowawezesha kusoma kwa utulivu zaidi na kuongeza umakini katika masomo yao.

Sauti ya wanafunzi