Joy FM

Vyombo visivyokidhi vigezo kuondolewa ziwa Tanganyika

24 August 2023, 15:37

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mkoa wa Kigoma, Limezindua kampeni ya Operasheni Maboya katika ziwa Tanganyika, ili kubaini Boti zisizo na Vifaa vya Kusafiria Kwa Wavuvi na Abiria ili kuwachukulia hatua za kisheria.

Baadhi ya abiria wakiwa katika moja ya vyombo vinavyotumiwa kwa usafiri katika ziwa Tanganyika. Picha na Danieli Amando.

Na, Kadislaus Ezekiel

Afisa mfawidhi shirika hilo mkoa wa Kigoma Abedi Mwanga amesema, wataviondoa vyombo vyote visivyokidhi vigezo vya kufanya shughuli za usafirishaji katika ziwa Tanganyika.

Sauti ya Afisa mfawidhi Bw. Abedi Mwanga

Aidha ameongeza kuwa tayari elimu imetolewa kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri pamoja na wavuvi, hivyo hategemei kuona miongoni mwao wanavunja sheria ili kuhakikisha usalama kwa wasafiri na wasafirishaji.

Sauti ya Afisa mfawidhi Bw. Abedi Mwanga

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wavuvi Mwalo wa Katonga Athuman Juma, amesema kitendo hicho kinaongeza usalama kwa wavuvi, pamoja na kuomba elimu izidi kutolewa ili kutambua umuhimu wa kutumia boya.

Sauti ya Mwenyekiti Bw. Athumani Juma