Joy FM

Maafisa tabibu watakiwa kuwa na maadili ya kazi yao

9 September 2024, 13:08

Wahitimu katika chuo cha maafisa tabibu wilayani kibondo wakiwa kwenye mahafali, Picha na James Jovin

Vijana waliohitimu mafunzo ya uafisa tabibu katika chuo cha uafisa tabibu wilayani kibondo mkoani kigoma wameaswa kuwa waadilifu katika kuwatumikia wananchi.

Na James Jovin – Kibondo

Halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma inapanga kuongeza kozi mbali mbali za masomo katika chuo cha maafisa tabibu wilayani humo ili kusaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa watumishi na kuboresha Zaidi sekta ya afya.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Kibondo bw. Deocles Rutema wakati wa mahafari ya kwanza ya chuo cha maafisa tabibu yaliyofanyika mjini kibondo katika ukumbi wa IOM.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kibondo Bw. Deocles Rutema

Naye Dr. Sebastian Pima mganga mkuu wa jiji la Dodoma ambaye ndiye mwanzilishi wa chuo hicho ameipongeza halimashauri ya wilaya ya Kibondo na kuitaka kuendelea kuboresha chuo hicho kwa kuwa ndiyo halimashauri pekee nchini inayomiliki chuo cha maafisa tatibu na hivyo kuwa mfano bora kwa halimashauri nyingine.

Sauti ya Sebastian Pima mganga mkuu wa jiji la Dodoma ambaye ndiye mwanzilishi wa chuo cha utabibu kibondo

Aidha mkuu wa chuo cha maafisa tatibu wilayani Kibondo Dr. Fredrick Kilindo ameiomba halimashauri ya wilaya ya Kibondo kusaidia katika maeneo mbali mbali kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuboresha Zaidi chuo hicho

Sauti ya mkuu wa chuo cha maafisa tatibu wilayani Kibondo Dr. Fredrick Kilindo

Mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey mwagwaza alikuwa mgeni rasimi katika mahafari hiyo ya kwanza ya chuo cha maafisa tabibu wilayani Kibondo, ameutaka uongozi wa chuo hicho kuendelea kuwa na mawazo chanya ili kuendelea kukuza chuo hicho na hatimae kiwe chuo cha mfano kote nchini.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey mwagwaza

Chuo cha maafisa tabibu wilayani Kibondo kilichoanza rasimi mwaka 2021 kina jumla ya wanafunzi 243 wavulana wakiwa 168 na wasichana 75 huku kikiwa na uwezo wa kudahili wanacho Zaidi ya 100 kila mwaka