Joy FM
Joy FM
30 July 2026, 12:39

Katibu tawa wa Wilaya Kasulu Bi. Teresia Mtewele amwataka madiwani kuhakikisha wanatoa taarifa za miradi ya maendeleo inayotelelezwa kwenye maeneo yao ili wananchi waweze kuifahamu
Na Emmanuel Kamangu
Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu wametakiwa kuhakikisha wanajitahidi kutoa mrejesho kwa wananchi juu ya shuguli mbali mbali za maendeleo zinazotekelezwa na serikali ya awamu ya sita.
Amebainisha hayo katibu tawala wilaya ya kasulu Bi Teresia Mtewele kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isack Mwakisu katika kikao baraza la madiwan cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/26 ambapo amewasihi madiwani kujenga utaratibu wa kuzungumza na wananchi ili kutambua kazi nzuri za maendeleo zinazoendelea kufanywa na serikali katika kata zao.

Aidha Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kasulu Bw, Benjamini Charles amewataka madiwani wenzake kuendelea kushirikiana na wananchi kikamilifu katika kuhakikisha wanawaletea maedndeleo.
Kwa upande wao baadhi ya madiwani mmoja wao akiwa Bw, Edson Hanyuma wameipongeza serikali ya awamu ya sita kwanamuna inavyoendelea kutekeleza maendeleo katika kata mbali mbali za wilaya hiyo jambo linaloakisi utendaji kazi wa raisi Dkt samia Suruhu hasani katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kikao hiki cha mwisho cha baraza la madiwani kwa mwaka wa fedha 2025/26 kimetanguliwa na baraza taarifa za kila kata na kufuatiwa na baraza la Madiwani ikiwa ni sehemu ya kujadili shuguli mbali mbali za maedneleo zinazotekelezwa na serikali ndani ya halmashauri ya wilaya ya kasulu.