Joy FM

Madiwani Kasulu waomba TARURA kuboresha barabara

1 September 2026, 11:12

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza la Madiwani halmashauri ya Mji Kasulu. Picha na Hagai Ruyagila

Miundombinu ya barabara ni sehemu muhimu katika maendeleo ya nchi kwani hutumika kusafirisha watu, bidhaa na huduma kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Na Hagai Ruyagila

Madiwani wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma, wameiomba serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), kundelea kuboresha barabara za pembezoni mwa mji wa Kasulu ambazo zimekuwa na changamoto ya kupitika.

Madiwani hao wametoa ombi hilo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Halmashauri hiyo.

Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza la Madiwani halmashauri ya Mji Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Wamesema hali mbaya ya baadhi ya barabara imekuwa ikiwakwamisha wananchi kufanya shughuli zao za uzalishaji mali kwa wakati, ikiwemo usafirishaji wa mazao na huduma nyingine muhimu.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu Mbelwa Chidebwe, amemshauri Meneja wa TARURA kuongeza kasi ya kuboresha barabara katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo, ikiwemo barabara inayoelekea kwa mkuu wa wilaya hiyo, ili ziweze kupitika kwa urahisi.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu. Picha na Hagai Ruyagila

Kaimu Meneja wa TARURA wilaya ya Kasulu, Mhandisi Eric Laban, amekiri kuharibika kwa barabara nyingi katika halmashauri hiyo, lakini mpaka kufika mwezi wa tisa wakandarasi wataendelea na kazi.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mh, Antony Lukole amesisitiza utekelezwaji wa changamoto zote zilizowasilishwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl Vumilia Julius Simbeye. Picha na Hagai Ruyagila