Joy FM
Joy FM
8 May 2026, 15:55

Viongozi wa Serikali za mitaa na viongozi wa dini wametakiwa kushirikiana na Polisi katika kuhamasisha ulinzi shirikishi ili kudhibiti uhalifu kwenye jamii
Na Esperance Ramadhan
Kamishna wa Polisi Jamii Nchini CP Alex Mkama ameitaka jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutanzua na kuzuia vitendo vya uhalifu wa wahalifu ambavyo vinaendelea kutokea katika maeneo yao.
CP Mkama anetoa wito huo wakati wa kikao kazi kilichohusisha viongozi wa serikali za mitaa, vijiji, kata na viongozi wa dini Mjini Kigoma ambapo ameeleza kuwa ili kutimiza adhma ya kudumisha amani na usalama wa wananchi na mali zao ni muhimu ushirikiano uwepo kati ya polisi na wananchi.
Aidha CP Mkama amewahimiza wazazi na walezi kuwafundisha maadili mema watoto wao lakini pia kuwekeza muda mwingi wa kuhudumia familia kwani kutaepusha baadhi ya vitendo vilivyo kinyume na maadili.
Kwa upande wake, Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kigoma Mjini Sadick Kibwana amelipongeza jeshi la polisi kwa kufanya kazi kwa weledi katika kulinda amani ya mkoa wa kigoma na nchi nzima kwa ujumla.
Hata hivyo baadhi ya wenyeviti wa mitaa na vijiji wamesema kuwa wataendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha kuwa suala la ulinzi na usalama linakuwa limeimarika